﻿Ezra.
2.
Basi hawa ndio watu wa jimbo waliotoka uhamishoni, ambao Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amewachukua mateka hadi Babeli (walirudi Yerusalemu na Yuda, kila mmoja kwenye mji wake, 
wakiwa wamefuatana na Zerubabeli, Yeshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu na Baana): Orodha ya wanaume kati ya watu wa Israeli ilikuwa: 
wazao wa Paroshi 2,172 
wazao wa Shefatia 372 
wazao wa Ara 775 
wazao wa Pahath-Moabu (wa jamaa ya Yeshua na Yoabu) 2,812 
wazao wa Elamu 1,254 
wazao wa Zatu 945 
wazao wa Zakai 760 
wazao wa Bani 642 
wazao wa Bebai 623 
wazao wa Azgadi 1,222 
wazao wa Adonikamu 666 
wazao wa Bigwai 2,056 
wazao wa Adini 454 
wazao wa Ateri (kupitia Hezekia) 98 
wazao wa Besai 323 
wazao wa Yora 112 
wazao wa Hashumu 223 
wazao wa Gibari 95 
watu wa Bethlehemu 123 
watu wa Netofa 56 
watu wa Anathothi 128 
watu wa Azmawethi 42 
wazao wa Kiriath-Yearimu, Kefira na Beerothi 743 
wazao wa Rama na Geba 621 
watu wa Mikmashi 122 
watu wa Betheli na Ai 223 
wazao wa Nebo 52 
wazao wa Magbishi 156 
wazao wa Elamu ile ingine 1,254 
wazao wa Harimu 320 
wazao wa Lodi, Hadidi na Ono 725 
wazao wa Yeriko 345 
wazao wa Senaa 3,630 
Makuhani: wazao wa Yedaya (kwa jamaa ya Yeshua) 973 
wazao wa Imeri 1,052 
wazao wa Pashuri 1,247 
wazao wa Harimu 1,017 
Walawi: wazao wa Yeshua na Kadmieli (kupitia jamaa ya Hodavia) 74 
Waimbaji: wazao wa Asafu 128 
Mabawabu wa lango la Hekalu: wazao wa Shalumu, Ateri, Talmoni, Akubu, Hatita na Shobai 139 
Watumishi wa Hekalu: wazao wa Siha, Hasufa, Tabaothi, 
wazao wa Kerosi, Siaha, Padoni, 
wazao wa Lebana, Hagaba, Akubu, 
wazao wa Hagabu, Shalmai, Hanani, 
wazao wa Gideli, Gahari, Reaya, 
wazao wa Resini, Nekoda, Gazamu, 
wazao wa Uza, Pasea, Besai, 
wazao wa Asna, Meunimu, Nefusimu, 
wazao wa Bakbuki, Hakufa, Harhuri, 
wazao wa Basluthi, Mehida, Harsha, 
wazao wa Barkosi, Sisera, Tema, 
wazao wa Nesia na Hatifa. 
Wazao wa watumishi wa Solomoni: wazao wa Sotai, Hasaferethi, Peruda, 
wazao wa Yaala, Darkoni, Gideli, 
wazao wa Shefatia, Hatili, Pokereth-Hasebaimu na Ami. 
Watumishi wa Hekalu wote na wazao wa watumishi wa Solomoni 392 
Wafuatao walikuja kutoka miji ya Tel-Mela, Tel-Harsha, Kerubu, Adoni na Imeri, lakini hawakuweza kuthibitisha kwamba jamaa zao zilikuwa uzao wa Israeli: 
wazao wa Delaya, Tobia na Nekoda 652 
Kutoka miongoni mwa makuhani: Wazao wa Hobaya, Hakosi, Barzilai (mtu aliyekuwa amemwoa binti wa Barzilai, Mgileadi, naye akaitwa kwa jina hilo). 
Hawa walitafuta orodha za jamaa zao, lakini hawakuonekana humo, kwa hiyo waliondolewa kutoka kundi la makuhani kwa kuwa walihesabiwa kuwa najisi. 
Mtawala aliagiza kuwa wasile chochote miongoni mwa vyakula vitakatifu hadi kuwe kuhani atakayehudumu kwa Urimu na Thumimu. 
Jumla ya watu wote waliorudi walikuwa 42,360; 
tena zaidi ya hao walikuwepo watumishi wa kiume na wa kike 7,337; pia walikuwamo waimbaji wanaume na wanawake 200. 
Walikuwa na farasi 736, nyumbu 245, 
ngamia 435 na punda 6,720. 
Walipofika kwenye nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, baadhi ya viongozi wa jamaa walitoa sadaka za hiari kwa ajili ya kujenga upya nyumba ya Mungu katika eneo lake. 
Wakatoa kwa kadiri ya uwezo wao na kutia katika hazina darkoni 61,000 za dhahabu, mane 5,000 za fedha, na mavazi 100 ya ukuhani kwa ajili ya kazi hiyo. 
Makuhani, Walawi, waimbaji, mabawabu, na watumishi wa Hekalu waliishi katika miji yao wenyewe, pamoja na baadhi ya watu wengine, nao Waisraeli waliosalia waliishi katika miji yao. 
