﻿Zaburi.
87.
Zaburi ya wana wa Kora. Wimbo. Ameuweka msingi wake katika mlima mtakatifu; 
Bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. 
Mambo matukufu yanasemwa juu yako, ee mji wa Mungu: 
“Nitaweka kumbukumbu ya Rahabu na Babeli miongoni mwa wale wanaonikubali mimi: Ufilisti pia na Tiro, pamoja na Kushi, nami nitasema, ‘Huyu alizaliwa Sayuni.’ ” 
Kuhusu Sayuni itasemwa hivi, “Huyu na yule walizaliwa humo, naye Aliye Juu Sana mwenyewe atamwimarisha.” 
Bwana ataandika katika orodha ya mataifa: “Huyu alizaliwa Sayuni.” 
Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.” 
