﻿Zaburi.
23.
Yahwe ni mchungaji wangu; sita pungukiwa na kitu. 
Yeye hunilaza katika majani mabichi; huniongoza kando ya maji matulivu. 
Yeye huurejesha uhai wangu; huniongoza katika njia iliyo sahihi kwa ajili ya jina lake. 
Hata ijapokuwa nikipita katika bonde la uvuli na giza nene, sitaogopa kudhurika kwa kuwa wewe uko pamoja nami; fimbo yako na gongo lako vya nifariji. 
Wewe waandaa meza mbele yangu katika uwepo wa maadui zangu; umenipaka mafuta kichwa changu na kikombe changu kinafurika. 
Hakika wema na uaminifu wa agano vitaniandama siku zote za maisha yangu; nami nitaishi katika nyumba ya Yahwe milele! 
