﻿Zaburi.
67.
Mungu atuhurumie sisi na kutubariki na kufanya nuru ya uso wake ituangazie Selah 
ili kwamba njia zako zijulikane nchi yote, wokovu wako kati ya mataifa yote. 
Watu wakusifu wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. 
Oh, mataifa wafurahi na na kuimba kwa furaha, maana utawahukumu watu kwa haki na kuwaongoza mataifa walioko duniani. 
Watu wakushukuru wewe, Mungu; watu wote wakusifu wewe. 
Nchi imetoa mavuno yake na Mungu, Mungu wetu, ametubariki. 
Mungu ametubariki sisi, na miisho yote ya dunia itamuheshimu yeye. 
