﻿Zaburi.
110.
Yahwe humwambia bwana wangu, “Kaa mkono wangu wa kuume mpaka nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.” 
Yahwe atainyosha fimbo ya nguvu yako toka Sayuni; utawale kati ya adui zako. 
Siku ile ya uweza wako watu wako watakufuata wakiwa katika mavazi matakatifu ya hiari yao wenyewe; tokea tumbo la alfajiri ujana wako utakuwa kwako kama umande. 
Yahwe ameapa, na hatabadilika: “Wewe ni kuhani milele, baada ya namna ya Melkizedeki.” 
Bwana yuko mkono wako wa kuume. Siku ile ya hasira yake atawaua wafalme. 
Yeye atahukumu matifa; ataujaza uwanja wa vita kwa maiti; atawauwa viongozi kaitka nchi nyingi. 
Atakunywa maji ya kijito njiani, kisha baada ya ushindi atainua kichwa chake juu. 
