﻿Zaburi.
114.
Israeli ilipotoka Misri, na nyumba ya Yakobo toka kutoka katika wale watu wa kigeni, 
Yuda ilifanyika kuwa mahali pake patakatifu, Ufalme wa Israeli. 
Bahari iliona ikakimbia; Yordani ilirudi nyuma. 
Milima iliruka kama kondoo waume, vilima viliruka kama wana-kondoo. 
Ewe Bahari kwa nini ulikimbia? Yordani kwa nini ulirudi nyuma? 
Milima, kwa nini uliruka kama kondoo waume? Enyi vilima wadogo, kwa nini mliruka kama wana-kondoo? 
Tetemeka, ee nchi, mbele za Bwana, uweponi mwa Mungu wa Yakobo. 
Aligeuza mwamba kuwa ziwa la maji, jiwe gumu kuwa chemchem. 
