﻿Zaburi.
128.
Amebarikiwa kila mtu amchaye Yahwe, atembeaye katika njia zake. 
Kazi ya mikono yako, wewe utaifurahia; utabarikiwa na kufanikiwa. 
Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao katika nyumba yako; wanao watakuwa kama miche ya mimea ya mizeituni wakaapo kuzunguka meza yako. 
Ndiyo, hakika, mtu anaye muheshimu Yahwe atabarikiwa. 
Mungu na akubariki toka Sayuni; na uweze kuona mafanikio ya Yerusalemu siku zote za maisha yako. 
Uishi uwaone wana wa wanao. Amani iwe na Israli. 
