﻿Zaburi.
150.
Msifuni Yahwe. Msifuni Yahwe katika patakatifu pake; msifuni katika mbingu za ukuu wake. 
Msifuni yeye kwa matendo yake makuu; msifuni yeye kwa kadri ya wingi wa ukuu wake. 
Msifuni kwa mlipuko wa pembe; msifuni kwa kinanda na kinubi. 
Msifuni kwa ngoma na kucheza; msifuni kwa vyombo vya nyuzi na filimbi. 
Msifuni kwa matoazi yavumayo; msifuni kwa matoazi avumayo sana. 
Kila kilicho na pumzi kimsifu Yahwe. Msifuni Yahwe. 
